Spika wa bunge Job Ndugai amesema kutokana na ripoti nyingi za ufisadi kuwahusisha viongozi mbalimbali wa siasa wakiwemo wabunge waliowahi kuwa mawaziri, ipo haja ya kuandikia barua vyama vyao ili visiwapitishe kugombea.
Hayo ameyasema leo Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti mbili za bunge kwa Rais Magufuli.
"Vyama vya siasa vina nguvu sana ipo haja ya kuviandikia barua, kwa sababu wananchi hawana makosa kuwachagua kwa sababu hawajui" ,amesema Ndugai.