Picha: MWANA HABARI NGULI MUHINGO RWEYEMAMU AZIKWA JIJINI DAR ES SALAAM

Roseline Rweyemamu (katikati) ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu, akiweka shada la Ua juu ya Kaburi la mumewe wakati maziko katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Watoto wa Marehemu, Muhingo Rweyemamu ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA NA VENANCE NESTORY
Wakuu wa Wilaya Wastaafu, wakiweka Shada la Ua juu ya Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu wakati wa maziko katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu (wa pili kushoto), akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani (TASWA0, Juma Pinto wakati wa shughuli ya kumuaga mwanahabari mkongwe,marehemu Muhingo Rweyemamu. Kulia ni Benny Kisaka na kushoto ni Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula
Sehemu ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili wa marehemu Rweyemamu
Wanahabari wakirekodi tukio hilo

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Mtanzania, ambaye pia alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Muhingo, akitoa salamu za rambirambi
Mtoto wa marehemu Muhingo, Emmanuel akisoma wasifu wa marehemu babake
Wajumbe wa kamati ya mazishi ya marehemu, Muhingo, wakijadiliana jambo wakati wa kuuaga mwili. Kutoka kushoto ni Joyce Mmasi, Mgaya Kingoba, Theophil Makunga, Abubakar Liongo na Benjamin Thomson
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk, Harrison Mwakyembe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhingo kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Muhingo
Sophia Mjema akimfariji mjane wa Muhingo, Roseline
Mkuu wa Wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akimfariji mjane wa marehemu Muhingo, Rweyemamu
Waombolezaji wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu,Muhingo
Mpigapicha wa zamani wa Daily News, Athuman Khamisi akimfariji mjane wa marehemu, Roseline
Baadhi ya wanahabari wakitoa heshima za mwisho, mbele ni Nyaronyo Kicheere
Wanahabari wakitoa heshima za mwisho
Mama mkwe wa marehemu, Muhingo, akilia baada ya kutoa heshima za mwisho
Roseline Rweyemamu (katikati) ambaye ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na Mwanahabari Mkongwe, akiugusa mwili wa mumewe wakati wa kuaga.
Waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari Mkongwe, Muhingo Rweyemamu baada ya kuutolea heshima za mwisho kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post