Picha: MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AZINDUA TAMASHA LA JINSIA MWAKA 2017 VIWANJA VYA TGNP MTANDAO MABIBO JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Septemba 5,2017 amezindua tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2017 lilirotaribiwa na TGNP Mtandao na Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia (GTI).



Tamasha hilo la siku nne linafanyika kuanzia Septemba 5 hadi 8,2017 katika Viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam huku mada kuu ikiwa ni “ Mageuzi ya Mifumo Kandamizi Kwa Usawa wa Kijinsia na Maendeleo Endelevu”.



Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mheshimiwa Samia Suluhu alisema serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika kuchangia kuharakisha maendeleo ya nchi.



“Serikali kwa kushirikiana na na wadau mbalimbali tumechukua hatua za maksudi ili kuhakikisha tunajenga jamii yenye usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kama ilivyoainishwa katika mikataba na maazimio mbalimbali ya kimataifa”,alieleza Suluhu.


Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi,kusimamia utekelezaji wa mipango na mikakati ya kuhakikisha wanawake na wanaume wanashiriki kwa usawa katika kujiletea maendeleo pamoja na kunufaika na maendeleo hayo.

Mheshimiwa Suluhu alitumia fursa hiyo kuwaasa wanawake kupendana,kunyanyuana,kufahamishana na kuelimishana na kupigania haki zao kwa kuzingatia mila na desturi zao.

Aidha aliipongeza TGNP kwa harakati zake za kuiunga mkono na kuikosoa serikali pale wanapoona imekwenda tofauti. 

Alisema kitendo cha kukemea na kutoa mapendekezo na suluhisho sehemu ambayo wanaamini serikali haijafanya vizuri ni kitendo cha kiungwana na kinachochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Aidha alizipongeza halmashauri za wilaya zinatoa asilimia 5 ya wanawake huku akiwataka wazazi kutumia fursa ya elimu bure kupeleka watoto wao shule ambapo takwimu zinaonesha kuwa kuna ongezeko kubwa la watoto wa kike waliopelekwa shule mwaka huu.

Mbali na uzinduzi huo ameongoza zoezi la kutoa tuzo kwa baadhi ya akinamama waliofanya vizuri na kutoa mchango katika maendeleo ya wanawake.

Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema Tamasha la Jinsia ni Jukwaa la wazi la wanawake na wadau wa haki za binadamu ambalo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja likiratibiwa na TGNP Mtandao lengo likiwa ni kushirikishana mafanikio,uzoefu,kuainisha changamoto na kuweka mkakati wa kukabiliana na changamoto hizo.

Liundi alibainisha kuwa Tamasha hilo linalofanyika kila mara baada ya miaka miwili linaandaliwa na taasisi kadhaa zinazotetea haki na usawa wa jinsia zikiongozwa na TGNP Mtandao na mwaka huu limeshirikisha wanawake zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

Aliongeza kuwa tamasha hilo linajikita katika kutambua mchango wa wanawake ambao wamekuwa mfano katika kuchochea maendeleo katika ngazi ya kitaifa na kimataifa lakini pia wanaume ambao wamekuwa mfano katika kutetea ajenda ya haki za wanawake.

“Malengo ya Tamasha hili ni kutafakari na kusherekea mafanikio,kujadili changamoto na kuweka mikakati ya pamoja kutatua changamoto hizo,kutathmini ushiriki wa wanawake katika michakato ya kufanya maamuzi na katika ngazi ya uongozi",alifafanua Liundi.

"Malengo mengine ni kufuatilia,kuhifadhi, kutambua na kusherekea viongozi wanawake wenye michango ya kuigwa juu ya usawa wa kijinsia na uwezo wa wanawake hususani Mapambano dhidi ya mfumo dume na kuimarisha harakati na nguvu za pamoja katika Ukombozi wa mwanamke”,aliongeza Liundi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule aliwataja na kuwapongeza wanawake waliofanya vizuri maeneo mbalimbali ambapo Makamu wa Rais alikabidhi tuzo kwa akina mama hao.

Miongoni waliopokea tuzo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu, aliyekabidhiwa tuzo yake na Mwenyekiti wa bodi.

Wengine ni pamoja na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda, Mbunge wa Bunda Mjini, Estar Bulaya, Mama Getrude Mongela, Dk. Ester Mwaikambo, na Msanii Fatma Baraka (Bi. Kidude) kwa jitihada walizozionesha katika uongozi na wote walipewa tuzo. 

Tamasha hilo limeandaliwa na mashirika mbalimbali ya wanawake na haki za binadamu,watu binafsi na wadau wengine wakiwemo Wanaharakati Vijana (YFF),Mtandao wa wanawake na Maji,Wanasemina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) na Vituo vya Taarifa na Maarifa.

Habari imeandaliwa na Kadama Malunde


ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI HAPA CHINI

Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (mwenye mtandio) akikata utepe pamoja na wageni meza kuu kuashiria uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.-Picha zote na Godwin Francis na Joachim Mushi.

Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (mwenye mtandio) akikata utepe pamoja na wageni meza kuu kuashiria uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.


Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi (kushoto) akimpongeza Spika mstaafu mwanamke wa Bunge la Tanzania, Anna Makinda (kulia) mara baada ya kupokea tuzo yake.Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo Mama Getrude Mongela (kulia) 

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017. 

Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.


Washiriki mbalimbali katika tamasha hilo.

Wawakilishi wa nchi mbali mbali wakitoa salam zao katika tamasha hilo

Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.Wa kwanza kushoto ni Happy Severine kutoka mkoa wa Simiyu akifuatiwa na Kadama Malunde kutoka mkoa wa Shinyanga na Grace Mwakalinga kutoka mkoa wa Mbeya

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Bi. Siaba Mkinga akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha hilo.

Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akizungumza leo wakati akizinduwa rasmi Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017. Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akizungumza leo wakati akizindua rasmi Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017. Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni wageni waalikwa meza kuu.


Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akicheza na wasanii na wageni waalikwa. 

Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marjorie Mbilinyi (kulia)

Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Zipora Shekilango (kulia) kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marry Lusimbi (kulia) kwenye uzinduzi rasmi wa Tamasha la Jinsia Tanzania la mwaka 2017.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mwakilishi wa halmashauri ya Kishapu Stephen Magoiga kwa kufanikiwa kutenga rasilimali fedha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 kuwezesha wasichana upata taulo za kujihifadhi bure wanapokuwa kwenye hedhi wakiwa shuleni.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi tuzo mwakilishi wa halmashauri Kisarawe.





 

Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kushoto) akikabidhi daktari wa kwanza mwanamke Tanzania, Dk. Ester Mwaikambo (kulia).



Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akitembelea miradi mbalimbali na shughuli za akinamama wanaharakati ngazi ya jamii za kujikwamua.


Washiriki wa Tamasha la 14 la TGNP Mtandao wakiwa katika tamasha hilo kwenye viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam
Wanawake washiriki wa Tamasha hilo wakicheza kwa furaha 
Wanawake washiriki wa tamasha la TGNP wakiwa katika tamasha hilo.
Baadhi ya washiriki wa tamasha la 14 la mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP mtandao) wakiwa katika tamasha hilo 
Wageni kutoka nchi mbali mbali 
Wanahabari wakifuatilia tamasha hilo 
Wanahabari wamiliki wa blog,Kadama Malunde na Joachim Mushi wakibadilishana mawazo 
Wanahabari kutoka mikoani walioshiriki tamasha hilo

Picha zote na Joachim Mushi na Francis Godwin

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post