MAKAMU MKUU WA CHUO CHA DAR ES SALAAM PROF.RWEKAZA MKANDALA ATUMBULIWA KWA UFISADI MLIMANI CITY

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) limemtimua Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Prof.Rwekaza Mukandala na watendaji wake kwa tuhuma za ufisadi katika mradi wa jengo la Mlimani City.


Kufuatiwa na tuhuma hizo zilizohakikiwa na mdhibiti mkakuguzi mkuu hesabu ya Serikali (CAG), mkataba mradi wa Mlimani City unatarajiwa kufumuliwa baada ya kubainika kuwa na kasoro nyingi zikiwemo chembechembe za ufisadi.


Aidha Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka amesema Prof. Mkandala amekiuka taratibu za ujibuji mashtaka mara baada ya kujibu hoja za sakata hilo la upigaji lililodumu kwa takribani saa 50 hadi 85 mbele ya kamati bila kumshirikisha mwenyekiti wa baraza la chuo.


Matiang’i: Bweni la wanafunzi liliteketezwa makusudi


Hivyo Mwenyekiti wa PAC amesema kamati yake imeguswa na taarifa ya CAG Kuhusiana na dalili za upigaji huo wa kudumu hivyo watahakikisha mkataba huo unafumuliwa na kurekebishwa ili uwe na manufaa kwa pande zote mbili.


‘’Mpaka wiki hii inamalizika tutakuwa tumeshapata taarifa kutoka kwa CAG ya jinsi gani utakuwa umerekebishwa ili uwe na manufaa kwa pande zote mbili’’.Amesema Kaboyoka.


CHANZO: Magazeti ya Tanzania leo Septemba 5, 2017
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post