Picha: MATUKIO YALIYOJIRI SIKU YA PILI KWENYE TAMASHA LA JINSIA MWAKA 2017 JIJINI DAR ES SALAAM


Tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2017 lilirotaribiwa na TGNP Mtandao na Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia (GTI) limeendelea leo Jumatano Septemba 6,2017 katika Viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.

Tamasha hilo limeanza Septemba 5 litaendelea hadi Septemba 8,2017, linaongozwa na mada “ Mageuzi ya Mifumo Kandamizi Kwa Usawa wa Kijinsia na Maendeleo Endelevu”.

Tamasha la Jinsia mwaka 2017  limefunguliwa rasmi jana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na linahudhuriwa na wanawake zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Nimekuwekea hapa matukio katika picha yaliyojiri leo Septemba 6,2017.
Mkurugenzi Idara ya Kuondoa Umaskini Wizara ya Fedha na Mipango Anna Mwasha  akiwasilisha mada ambapo amewataka Watanzania wakiwemo akina mama kuunda vikundi mbalimbali ili kupewa mikopo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Mratibu wa Ardhi kutoka Shirika la Care International Marry Ndaro akiwasilisha  mada ambapo amezungumzia masuala ya umiliki wa ardhi kwa wanawake sera  inapaswa kutoa kipaumbele kwa mwanamke ili aweze kumiliki ardhi.
Mratibu wa Masuala ya Ujumuishwaji kutoka shirika la Sight Savers Angela Michael akiwasilisha dada katika tamasha hilo.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bengi Issa  akiwasilisha Mada katika Tamasha la Jinsia 2017. 
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi akichangia mada katika tamasha hilo ambapo amesema bila mwanamke kumiliki ardhi bado suala la  kukua kiuchumi kwa mwanamke ni changamoto kubwa hususani maeneo ya vijijini.
Siti Abbas Ali kutoka Shirika la Zanzibar Coalition akichangia mada ambapo  amesema wanamke wa Zanzibar wanakumbwa na changamoto katika  kuchagua na kuchaguliwa ngazi za uongozi.
Washiriki katika tamasha hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia matukio katika tamasha hilo.
Baadhi ya Viongozi Wanawake akiwemo aliyekuwa Spika wa Bunge Anna Makinda,  Esther Bulaya wa pili kutoka Kulia wakieleza jinsi walivyodhubutu kama  wanawake ni katika majadiliano ambayo yameandaliwa na TGNP Mtandao 
katika tamasha hilo la Jinsia 2017.

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya akieleza alivyodhubutu kama mwanamke na kuweza kuchaguliwa na wananchi bila kujali mila na desturi.
Picha zote na Frankius Cleophace wa Cleo24 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post