WAZIRI NCHEMBA ATISHIA KUWAFUTIA URAIA WATANZANIA WENYE UBAGUZI

Waziri wa mambo ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba ametishia kuwafutia uraia watanzania wapya wa Katumba mkoani Katavi ambao walikuwa wakimbizi kwa muda mrefu kutokana na tabia ya ya baadhi yakubaguana kitaifa na kikanda.


Waziri Nchemba amesema hayo jana wakati alipopita kwenye kambi kuangalia usajili unaendeleaje ambapo amesema wananchi hao waliopewa uraia wakitokea burundi wakati wa vita ya kikabila miaka 1972 wamekuwa na tabia ya ubaguzi hata kufikia kushindwa kusaidiana kwenye biashara zao.


Waziri aliwaambia wananchi hao kuwa yeyote atakayeleta mambo ya ubaguzi ikiwa ni pamoja na kubaguana kibiashara katika jamii hatosita kumfutia uraia alioupata kwani Watanzania hawana mambo ya kibaguzi.


Pamoja na hayo Kiongozi huyo alitumia muda huo kuwataka Watanzania kuwa na utanzania ndani ya mioyo yao na waache tabia ya kutaka kukwamisha kila kitu kinachofanywa na serikali kwa kuweka vikwazo mbele ili vitu visifanikiwe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post