TAKUKURU: SETHI HANA SIFA YA KUTIBIWA NJE YA NCHI WALA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ leo August 3, 2017 imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi hatotibiwa nje ya nchi wala Hospitali ya Muhimbili, bali atatibiwa Hospitali ya Amana na Lugalo.


Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa Sethi hana sifa ya kutibiwa nje ya nchi wala Hospitali ya Taifa Muhimbili, bali ni Amana na Lugalo ambapo kuna ulinzi na usalama.


Aidha, Swai ambaye amedai watampeleka Sethi Hospitali ndani ya siku 14, ameyaeleza hayo baada ya Wakili wa utetezi, Alex Balomi kudai kwamba hadi sasa Sethi hajapewa matibabu licha ya Mahakama kuamuru atibiwe.


Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Shaidi alisema hakutoa amri ya Sethi kutibiwa nje ya nchi, bali alitoa amri ya kutibiwa ikiwezekana Muhimbili, hivyo ameutaka upande wa mashtaka kuhakikisha ndani ya siku 14 mshtakiwa anapatiwa matibabu ambapo kesi imeahirishwa hadi August 17, 2017.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post