Picha : DC SHINYANGA AZINDUA MRADI WA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA UNAOTEKELEZWA NA TVMCMkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia.
***

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro amezindua mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia ‘GBV Prevention Project’ unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Agosti 14,2017 katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake na watoto  wakiwemo wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali,maafisa watendaji wa kata,maafisa tarafa,afisa maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii,afisa utamaduni na dawati la jinsia na watoto.

Akizungumza wakati wa kuzindua mradio huo,Matiro alilipongeza shirika hilo kwa kuelekeza nguvu zake katika mapambano dhidhi ya ukatili wa kijinsia ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii husika kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wahusika wanapobainika.

“Serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali,ili mfanikiwe mnatakiwa mshirikishe wadau kwenye maeneo husika,mmefanya jambo jema kujitambulisha badala ya kuanza kutekeleza mradi kimya kimya kama baadhi ya mashirika vile yamekuwa yakifanya hali inayowafanya washinde kufanikiwa”,alieleza Matiro.

“Serikali ipo nanyi bega kwa bega,pale mnapokwama tafadhali tupeni taarifa nasi tutawasaidia kadri tutakavyoweza kwani lengo kuu ni kuwahudumia wananchi wetu ili kuzuia vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa wanawake na watoto katika jamii”,aliongeza Matiro.

Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuyakumbusha mashirika na taasisi mbalimbali zinazotekeleza miradi katika jamii kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la jadi ‘sungusungu’,viongozi wa kimila pamoja na watu mbalimbali wenye ushawishi katika jamii husika.

Akitambulisha Mradi huo,Mkurugenzi wa TVMC,Mussa Jonas Ngangala alisema mradi huo unaofadhiliwa na taasisi ya kusaidia asasi zisizokuwa za kiserikali la The Foundation For Civil Society unaolenga kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia utatekelezwa katika kata tano katika wilaya ya Shinyanga ambazo ni Usanda,Samuye,Nsalala,Tinde na Didia.

Ngangala alisema ili kutekeleza mradi huo kikamilifu shirika hilo litashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo viongozi serikali,dini,wananchi na wadau wengine.

“Matarajio yetu kupitia mradi huu ni kwamba kufikia mwezi Januari mwaka 2018 kuwepo na mfumo mzuri wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kutoka ngazi ya jamii hadi dawati la jinsia kwa kushirikiana na maafisa utamaduni,maafisa watendaji,maafisa maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii na mashirika mengine”,alieleza Ngangala.

“TVMC ambayo walengwa wake wakuu ni watoto na wanawake imekuwa ikishirikiana na serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha watoto wanapata ulinzi na usalama ,elimu na afya bora,msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto lakini pia matunzo kwa watoto”,alieleza Ngangala.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud alisema kupitia mradi huo wataibua mijadala kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia kupitia matamasha,michezo,ngoma za asili,kutoa elimu na mbinu zingine kadha wa kadha.

Katika hatua nyingine Daud alisema ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoani Shinyanga ni vyema wadau wote wakashiriki katika mapambano hayo badala ya kuiachia serikali pekee.

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud,kushoto ni Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza ukumbini. 
Wadau wa haki za watoto na wanawake wakiwa ukumbini. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia. 
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
Mkurugenzi wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akitambulisha mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na shirika hilo.
Wadau wakiandika dondoo muhimu.
Mkurugenzi wa TVMC ,Mussa Jonas Ngangala akitambulisha mradi huo.
Wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa mradi huo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mkurugenzi wa TVMC ,Mussa Jonas Ngangala akisisitiza jambo ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akielezea kuhusu mbinu mbalimbali watazozitumia katika kufanikisha mradi huo.
Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
Kiongozi wa dawati la Jinsia na watoto Shinyanga,Vivian Zabron akichangia hoja wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia. 
Wadau wakiwa ukumbini. 
Afisa Utamaduni wilaya ya Shinyanga,Janeth Elias akichangia hoja ukumbini. 
Wadau wakiwa ukumbini. 

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post