MWANAUME AFARIKI BAADA YA KUPIGA KURA KENYA


Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Patrick Odoyo amepoteza fahamu na kufariki masaa matano baada ya zoezi la upigaji kura kuanza, katika eneo la Nyando Kisumu nchini Kenya.

Patrick Odoyo ambaye alikuwa mtu wa tano kupiga kura katika kituo cha kata ya Kobura, alipoteza fahamu na kisha kukimbizwa kituo cha afya cha Ahero ambako mauti ilimkuta, na mwili wake kuhifadhiwa katika chumba cha maiti.

Mpaka sasa haijajulikana sababu ya mtu huyo kupoteza fahamu na kufariki, lakini vyanzo vya habari vimeeleza kuwa watu wengi wametoka nyumbani alfajiri kuwahi kupiga kura bila kula kitu chochote, na hali mbaya ya hewa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post