MWALIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mwalimu wa shule ya msingi katika kata ya Ligunga tarafa ya Matemanga wilaya Tunduru mkoani Ruvuma Rajabu Morisi amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake na kumsababishia ujauzito.


Akisoma shauri hilo no 148/2017, mbele ya mlinzi wa amani hakimu wa Mahakama ya mwanzo Itika Korosho, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya wilaya Inspekta Bosco Kilumbe amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya mwezi January na Mei mwaka huu katika muda usiojulikana baada ya kumrubuni mwanafunzi huyo.


Na kudai kufanya hivyo ni kinyume cha sheria namba 130 (1) na (2e) na namba 131 (1) na (2) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


Hata hivyo mtuhumiwa huyo amekana kosa hilo upelelezi bado unaendelea , mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana, kesi hiyo itatajwa tena Mahakamani Agosti 28 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post