MKOJO WA MANJI WAENDELEA KUZUNGUMZIWA MAHAKAMANI

Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic ameieleza Mahakama ya Kisutu leo August 23, 2017 kuwa dawa za kulevya (Benzodiazepines) alizobainika anatumia mfanyabiashara Yusuf Manji zinatolewa hospitalini na zinauzwa Pharmacy.


Mkemia huyo amesema hajui kama sampuli ya mkojo alioupima ni wa Manji ama Askari Polisi, kwa sababu wakati Manji anachukuliwa sampuli hiyo aliingia chooni na Askari, huku yeye akiwasubiri nje.


Aidha, Mkemia amesema katika kipimo cha mkojo wa Manji amebaini uwepo wa dawa aina ya Benzodiazipines ikiwa ni zao la Heroin, ambapo dawa hiyo ina matumizi mengi ikiwemo kuondoa maumivu makali, ikitegemeana na ushauri wa daktari.


Baada ya kuelezwa hayo, Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis amesema Serikali imefunga ushahidi wa mashahidi wake watatu.


Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema atatoa uamuzi kama Manji ana kesi ya kujibu ama la, August 25/2017.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post