MBUNGE WA ZAMANI WA UKONGA NA SEGEREA DK.MAKONGORO MAHANGA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.


Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni.


Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”.


Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi.


Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527