Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana amefunguka na kusema kuwa hakuna Rais duniani kote ambaye awewahi kuja Tanzania mara nyingi na mkoa wa Tanga kama Rais Museveni.
Kinana amesema hayo leo katika sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta katika eneo la Chongoleani Tanga na kusema kuwa Museveni ni ndugu yetu na si rafiki wa Tanzania.
“Hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanzania mara nyingi kama Museveni, hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanga mara nyingi kama Museveni, alikuwa akitusihi sana kujenga reli hapa Tanga ila leo naona anafuraha kwamba reli haikuwezekana lakini bomba la mafuta limeonekana, lakini nampongeza sana Rais Magufuli kwa sera zao nzuri na vyama vyao kuwezesha bomba la mafuta” alisema Kinana na kuongeza;
“Nimemsikia Museveni akisema Tanzania na Uganda ni nchi ndugu na si marafiki, naona Rais Magufuli na Museveni wote wanasema siasa ni uchumi na uchumi ni siasa” alisema Kinana
Aidha Rais wa Uganda Museven amesema kuwa Watanzania ni ndugu zake kabisa ila wazungu wote kwake ndiyo marafiki
“Mimi siwezi kusema Watanzania rafiki hapana ni ndugu zangu, mkinikubali nafurahi hata msiponikubali mimi nitabaki kuwa ndugu yenu, hao watu weupe (Wazungu) ndiyo wabaki kuwa marafiki” alisisitiza Museveni