KIKWETE AMVAA WAZIRI WA MAGUFULI


Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amemvaa Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Khamis Kigwangala na kumwambia anaweza kuwa sehemu ya wachochezi kwa anachokifanya.


Ridhiwani Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya Mhe. Kigwangalla kuonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma katika kuwafanyia usaili baadhi ya wataalamu waliojitokeza kwenye usaili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao umefanyika mapem jana Agosti 30, 2017.


"Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakuwa sehemu ya wachochezi! Mhe. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lakini picha inatoa jibu sahihi", aliandika Ridhiwani.


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Agosti 30, 2017 ilifanya usaili kwa ajili ya nafasi za kazi katika Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo takribani watu 30,000 walijitokeza huku ikiwa watu 400 pekee ndiyo wanaotakiwa.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527