Picha: WATU WATATU WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA WIZI WA PIKIPIKI KAHAMA



Wananchi waliojichukulia sheria mkononi leo wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki. 

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yamefanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa leo majira ya saa nne asubuhi.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili waliouawa leo baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.

Afisa mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.

Miili ya marehemu hao imechukuliwa na Jeshi la polisi wilaya ya Kahama, na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitwana,Peter Joseph akiwa katika eneo ambalo watu hao wamechomwa moto
Nyumba ya mmoja wa watuhumiwa ikiendelea kuwaka moto,katikati ni pikipiki iliyokutwa kwenye shimo la choo ikichomwa.
Baadhi ya waendesha boda boda na wananchi wakiwa katika eneo la makazi ya mmoja wa watuhumiwa wakishuhudia nyumba ikiteketea.
Mkuu wa polisi wilaya ya kahama Mussa Mchenya mwenye kofia nyeusi akiwa eneo la tukio akishuhudia eneo ambalo watuhumiwa hao wamechomewa moto.
Wananchi wakiwa katika makazi ya mtuhumiwa aliyechomwa moto wakishuhudia nyumba ikiteketea.
Nyumba ikiendelea kuteketea eneo la Sofia Kahama.
Baadhi ya waendesha bodaboda na wananchi wakiangalia nondo iliyochongwa ambayo inahisiwa kutumika katika mauaji ya madereva boda boda.
Afisa wa jeshi la polisi akiendesha pikipiki ya mmoja wa mwendesha boda boda ambayo alikutwa eneo la tukio na kukamatwa kwa lengo la kusaidia polisi.
Maafisa wa polisi wakiwa eneo la tukio
Shimo ambalo mtuhumiwa inadaiwa alificha pikipiki tatu ndani yake.
Wananchi wakiendelea kubomoa nyumba ya mtuhumiwa

Askari polisi wakiwa katika eneo la tukio baada ya kuchukua miili ya watuhumiwa waliochomwa moto.
Maafisa wa polisi wakiwa wameifikisha miili ya watuhumiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Picha zote na mwandishi wa Malunde1 blog - Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post