MBUNGE WA CHADEMA HALIMA MDEE AKAMATWA NA POLISI KWA AGIZO LA MKUU WA WILAYA

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza majira ya saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu leo Jioni Julai 4,2017.

Awali akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post