MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI ATAKA WANAOSAMBAZA VIDEO YA MCHELE WASHUGHULIKIWE

Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la upotoshaji na kuliagiza Jeshi la polisi kuanza mara moja kuwashughuliakia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wenye tabia hiyo.


Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi huyo mara baada ya mitandao ya kijamii kusambaza video yenye habari inayonyesha uwepo wa mchele wa plastiki nchini.


Boaz amekanusha uwepo wa mchele huo wa plastiki na kumsaka kwa udi na uvumba mtu aliyerekodi video hiyo ili asaidie kutoa taarifa zaidi.


Na amewaomba wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, kwani ni hatari na husababisha madhara makubwa katika jamii.


”Kabla ya kusambaza taarifa kwanza uwe na uhakika wa vyanzo vyako, wahsuika wanaweza kuingia kwenye matatizo yasiyokuwa ya msingi”. amesema Boaz.


Aidha waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na wazee na watoto , Ummy Mwalimu ametaarifiwa na Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), kuwa hakuna mchele wa aina hiyo nchini.


Waziri Ummy amewasisitizia watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, na kuepuka upotoshaji.

Hii ni Taarifa ya TFDA 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527