LIPUMBA AZIDI KUMKABA KOO MAALIM SEIF



Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amedai kuwa safari hii Maalim Seif Shariff Hamad amegota, huku akieleza kuwa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho imeagizwa kumhoji pamoja na wenzake, ili kujibu tuhuma za kukihujumu chama hicho.

Lipumba ameyasema hayo leo Julai 4,2017 jijini Dar es Salaam, na kudai kuwa Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, hatoweza kufanya kazi zake za chama hadi pale atakapokubali kurudi ofisini kwake na kumuomba radhi.

“Kazi zake zitafanywa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya hadi pale atakapo kuja ofisini na kuniomba radhi Mwenyekiti wake. Baraza Kuu la Uongozi limeagiza Kamati ya Maadili na Nidhamu kumhoji kwa nini anakihujumu chama, pia Nassoro Mazrui atahojiwa kwa nini anamnyanyasa bosi wake Sakaya sambamba na wabunge nao watahojiwa,” amesema.

Lipumba amedai kuwa, CUF iko katika kipindi cha marekebisho na kuwataka wanachama aliowaita wasaliti kujirudi.
Na Regina Mkonde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post