KIJANA ANUSURIKA KUFA KWA KICHAPO BAADA YA KUTAPELI KWENYE DUKA LA MPESA SHINYANGA MJINI


Kijana akiwa amekaa chini baada ya kutembezewa kichapo na wananchi

Kijana akijitetea


Kijana akiwa amepanda kwenye gari la polisi-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
****
Kijana mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja amenusurika kufa kutokana na kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kutapeli pesa shilingi 370,000/= katika kibanda cha duka la Mpesa katika soko la Kambarage kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.


Tukio hilo limetokea leo Julai 6,2017 majira ya saa nane mchana ambapo kijana huyo alifika kwenye kibanda cha Mpesa cha Robert Masesa kilichopo jirani na soko la Kambarage na kutapeli kiasi hicho cha pesa.

Akisimulia kuhusu mkasa huo mmiliki wa kibanda hicho, Masesa alisema majira ya saa tano kijana huyo alifika kibandani hapo akitaka huduma ya kutoa pesa ,lakini alipoombwa simu yake iangaliwe ujumbe mfupi wa maneno katika simu kama udhibitisho akawa hana simu.

Alisema alipommbana akasema ametumia namba ya mwingine ndipo akaagizwa amfuate ,lakini kabla hajaondoka akaja mteja mwingine kutoa pesa ndipo akanuti yake ikasema namba yake imefungiwa.

Masesa alieleza kuwa baada ya kupata ujumbe huo ,ndipo akashtuka kuwa ametapeliwa na alipomuita kijana huyo alianza kutimua mbio na baiskeli ndipo akapiga yowe na hatimaye kijana kunaswa na na wananchi kisha kuanza kupewa kichapo.

Hata hivyo wakati wananchi hao wakitembeza kichapo ndipo wakafika askari polisi na kumnusuru kutoka katika kichapo hicho ambacho kiliambatana na mawe makubwa na kuokoa uhai wake na kisha kuondoka naye kwenda kituo cha polisi.

Na Marco Maduhu-Malunde1 blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post