PSPF YAWAHAMASISHA WANACHAMA NA WANANCHI KUENDELEEA KUTEMBEELA BANDA LAO MAONESHO YA SABASABA 2017


Win-God Simon, (kushoto), Afisa wa PSPF akiwahudumia wananchi na wanachama wa Mfuko huo waliotembeela banda la PSPF leo Julai 6, 2017

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi(kulia), akipokea vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko wa Pensehni wa PSPF kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul
Njaidi wakati alipotembeela banda la Mfuko huo leo Julai 6, 2017.

****

MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaahidi wananchi wanaojitokeza kwenye banda la Mfuko huo, lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, kuwa wataendelea kupatiwa huduma zote kama ambazo wamezoea kuzipata kwenye ofisi za Mfuko huo kote nchini.


Ahadi hiyo imetolewa leo Julai 6, 2017 na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, baada ya kuona umati mkubwa wa wananchi waliofika kupatiwa huduma mbalimbali zikiwemo zile za wanachama kujua michango yao, wananchi kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), ambapo mtu aliyejiunga na mpango huo husajiliwa na kupatiwa kitambulisho papo kwa hapo.

 "Leo idadi ya watu imeongezeka sana bila shaka wamevutiwa na huduma zetu na tunawahakikishia tutaendelea kutoa huduma bora na za haraka hadi tarehe ambayo maonesho haya yatafikia kilele kama alivyoagiza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa siku za maonesho zimeongezeka hadi Julai 13, 2017 badala ya Julai 8",lifafanua Bw. Njaidi.

Idadi kubwa ya wananchi waliofika kwenye banda hilo ni wale wajasiriamali ambao wengi wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ambapo moja ya faida kubwa ya kujiunga na mpango huo ni kupata fao la bima ya afya inayomuwezesha mwanachama kupatiwa matibabu yeye na wategemezi wake kwenye hospitali zilizoaishwa kote nchini.

Wananchi waliofurika wkenye banda la PSPF, leo Julai 6, 2017
Bw. Costa wa PSPF, (kushoto), akifafanua jambo kwa wananchi hawa waliofika kwenye banda la PSPF
Afisa Michango wa PSPF, Bw. Noah Amri, (kushoto), na Afisa Uendeshaji anayeshughulikia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Bi. Asmahan H. Haji, wakiangalia taarifa kwenye kompyuta.
Afisa msaidizi wa uendeshaji Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Musa Mfaki(kushoto), akimuhudumia mwananchi
Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, (kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la PSPF

Afisa msaidizi wa uendeshaji Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Musa Mfaki, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Fatma Gulamali, baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), kwenye banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wiara ya Fedha na Mipango, viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba Julai 6, 2017. 
Wananchi waliofurika kwenye banda la PSPF, leo Julai 6, 2017

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post