HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA YATAKIWA KUTENGA BAJETI ILI KUINUA SEKTA YA KILIMO


Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Igunga, Peter Onesmo (kulia), akizungumza na waandishi wa habari na maofisa Ugani wa wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo maofisa Ugani wa wilaya hiyo kwenye kilimo cha mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi lishe yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kupitia Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB). Kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya hiyo, Erasto Konga na Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Shadrack Kalekayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Costa Ulomi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Bestina Daniel akizungumza wakati akielezea madhumuni ya mafunzo hayo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa wilaya hiyo, ambaye ni mtunza fedha, Gordon Dinda akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi.
Mwakilishi wa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mathias Mbogo akizungumza.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Bestina Daniel akizungumza wakati akielezea madhumuni ya mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora, Saidi Babu akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mshauri wa Matumizi ya Bioteknolojia kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange akitoa mada
Wanahabari wakiwa kazini. Kulia ni Gelard Kitabu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Kilimo na Benson.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Filbert Nyinondi akitoa maelekezo kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo. 
Maofisa Ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo. Kulia ni Athuman Mgunya na Dickson Kanyanka.
Maofisa ugani wakiwa katika mafunzo hayo. Kutoka kulia ni Emmanuel Raymond, Claudia Mlowe na Neema Kaduguda.
Mafunzo yakiendelea.
Maofisa ugani ndani ya mafunzo.
Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya hiyo, Erasto Konga, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Shadrack Kalekayo, akizungumza.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo wakiwa tayari kwa kazi. Kutoka kulia ni Bakar Josephat na Stellah Chirimi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru Mwanza,na Dk. Nicholaus Nyange kutoka Jukwaa la Bioteknolojia.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Taswira ya ukumbi wakati wa mafunzo hayo.
*****

HALMASHAURI ya Wilaya ya Igunga imeshauriwa kutenga bajeti katika bajeti zake za kila mwaka kwa ajili ya kuinua sekta ya kilimo wilayani humo.

Ushauri huo umetolewa na leo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Costa Ulomi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku ya kuwajengea uwezo maofisa Ugani wa wilaya hiyo kwenye kilimo cha mazao ya Mihogo, Pamba na Viazi lishe yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kupitia Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB).

"Napenda kumuomba Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya yetu anapo kutana na watendaji wake kutenga bajeti kwa ajili ya kuinua kilimo katika wilaya yetu" alisema Olomi.

Olomi alisema kuwa bila ya kuwa na bajeti iliyotengwa kwenye kilimo bado changamoto ya kuinua kilimo itaendelea kuwepo.

Aliongeza kuwa kilimo kipanda itasaidia kupata malighafi nyingi ambayo itatumika kwenye viwanda vinavyotarajiwa kuanzisha hapa nchini.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Peter Onesmo aliwataka maofisa ugani hao baada ya kupata mafunzo hayo kwenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi waliopo katika vijiji na Kata wanatoka.

"Nawaombeni haya mafunzo mtakayo yapata yasibaki kwenye makabrasha na kwenye makabati badala yake yapelekeni kwa wakulima ili kusaidia kuinua kilimo chenye tija katika wilaya yetu" alisema Onesmo.

Alisema kilimo chenye tija ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki cha nchi kuelekea kwenye uchumi wa viwanda ambapo kunahitaji kupatikana kwa mbegu bora na kufuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo.

Aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo yataanzishwa mashindano ya vijiji na kata ili kubaini ni kata gani imeweza kufanikiwa katika sekta ya kilimo na ipi imefanya vibaya na kwa kata itakayoshinda itapewa zawadi.

"Tunahitaji wilaya yetu iwe ya mfano katika sekta ya kilimo na uwezo huo tunao" alisisitiza Onesmo.

Akizungumza wakati akitoa mada kwa maofisa ugani hao kuhusu matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange alisema teknolojia hiyo imeleta mapinduzi ya kilimo kwa nchi ambazo imeanza kuitumia. 

Alitaja baadhi ya nchi ambazo zilianza tangu zamani kutumia teknolojia hiyo kuwa ni Amerika ya Kaskazini na Kusini, India, Pakistan, Afrika Kusini na Ulaya.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Costech,Bestina Daniel alisema mafunzo hayo ni moja ya utekelezajiwa kazi za COSTECH za kuwawezesha wakulima na wagani katika kutumia mbinu na teknolojia bora za kilimo kwenye uzalishaji ili kuongeza tija na kupunguza umasikini kwenye kaya.

Alisema Costech ndio wenye dhamani ya kuishauri Serikali kwenye masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia hivyo pale kunapotokea teknolojia na mbinu nzuri ambazo zinaweza kuleta mageuzi kwenye uzalishaji kwa wakulima hutafuta mbinu mbalimbali za kuzifikisha kwa wahusiaka.

Aliongeza kuwa ili kufikia kwenye uchumi wa viwanda lazima malighafi za kutosha ziwepo ili kulisha viwanda hivyo na kuzalisha bidhaa hivyo mazao hayo ambayo Costech inayahamasisha yatasaidia sana katika kulisha viwanda vya nguo,usindikaji wa mihogo na viazi lishe ambavyo vina umuhimu mkubwa kwenye kuongeza lishe na usalama wa chakula.

Na Dotto Mwaibale- Igunga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post