HATIMAYE ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU ANNA MGHWIRA KUTEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO



Zitto Kabwe

Rais Dk. John Magufuli jana amemteua Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, mwenyekiti huyo wa chama cha upinzani, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Said Meck Sadiki.

Baada ya kukaa kimya kufuatia uteuzi huo hatimayeLeo Jumapili June 4,2017 Kiongozi wa AICT Wazalendo Zitto Kabwe ametoa ujumbe yafuatayo:

"Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini. 

Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto,Mb 

Kiongozi wa Chama"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post