TANESCO YATOA OMBI KWA WANANCHI WOTE


SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa mapema mara inapotokea hitilafu ya umeme iliyosababishwa na mvua au sababu nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2017, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, sambamba na hilo pia wananchi wasifanye shughuli au kukaa chini ya miundombinu ya umeme.

“Lakini tunawaomba wananchi watoe taarifa haraka maeneo yenye mafuriko au mkusasnyiko wa maji mengi ili wataalamu wetu waweze kuchukua hatua za haraka.” Alisema.

Dkt. Mwinuka pia alisema endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi au alama ikawekwa ili kuwapa hadhari wapiti njia na watoto wasikaribie eneo hilo wakati mafundi wa TANESCO wakichukua hatua za marekebisho.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), katika taarifa yake iliyotoa Mei 9, 2017 imeonya kuwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba, yatakabiliwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Mei 10 hadi 12, 2017.

 Aidha kwa upande wake, mtaalamu wa masualaya umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Simon Kihiyo, amewahakikishia wananchi kuwa miundombinu ya TANESCO iko imara na salama, na hitilafu zinazotokea za hapa na pale nyingizinasababishwa na sababu za kibinadamu, au za kimazingira kama vile nguzo za umeme kugongwa na magari, au miti kuangukia nguzo. 

"Naomba nitoe angalizo kwa wateja wetu, kama pametokea hitilafu yoyote ya umeem nyumbani kwako, ni vema ukatoa taarifa TANESCO au ukamtafuta fundi wa umeme mwenye taaluma badala ya kushughulikia tatizo hilo wewe mwenyewe ilihali ukiwa huna utaalamu na masuala ya umeme, kwani hiyo ni hatari."

Naye kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji amesema, katika kipindi hiki cha mvua kuna athari ndogo ndogo zimetokea kwenye miundombinu ya TANESCO hususan nguzo za umeme, lakini akatoa hakikisho kuwa mafundi wa TANESCO wanekuwa wakichukua hatua za haraka kurekebisha athari katika miundombinu ya umeme pindi tu zinapotokea.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Me11, 2017. Dkt. Mwinuka ametoa hadhari kwa wananchi kutogusan miundombinu ya Tanesco hususan nyaya zilizoanguka, au kufanya shughuli yoyote karibu na miundombinu yab umeme katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendela kunyesha nchini. Kulia ni Mhandisi Simon Kihiyo, na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.


Mhandisi Simon Kihiyo, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu hatua za kuchukua pindi hitilafu ya umeme inapotokea

Dkt. Mwinuka (kushoto) na Mhandisi Kihiyo, wakati wa mkutano huo leo
Dkt. Mwinuka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, akitoaufafanuzi zaidi wa hatua za kuchukua endapo wateja au wananchi wataona hitlafu ya umeme kwenye maeneo yanayowazunguka
Mhandisi Kihiyo, (kulia0na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji katika mkutano na wanahabari
Mhandisi Simon Kihiyo, (kulia), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (kushoto) na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila wakijadiliana jambo.

Na K-VIS BLOG/Khalfan Said

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post