Makubwa Haya!! KUTANA NA KIWANDA KINACHOTENGENEZA BIA YENYE MKOJO WA BINADAMU

Mkojo huo ulikusanywa kutoka kwa hafla moja kubwa zaidi ya muziki barani ulaya miaka miwili iliyopita.

Kiwanda kimoja cha pombe nchini Denmak kimetengeneza bia mpya ambapo ngano huchanganywa na lita 50,000 za mkojo

Hata hivyo bia hiyo haitakuwa na mkojo wa binadamu.

Mkojo huo ulikusanywa kutoka kwa hafla moja kubwa zaidi ya muziki barani ulaya miaka miwili iliyopita

"Wakati habari kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe zilifichuka, watu walidhani kuwa tulikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja kuenda kwa pombe," alisema mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus.Bia hiyo haina ladha ya mkojo kabisa

"Kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu moja ambaye alihudhuria warsha hiyo ya muziki mwaka 2015.,

Lita hizo 50,000 zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa 60,000 za bia.

Mashine iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji, inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja mbolea ikitumia nguvu za miale ya jua.Mashini iliyotumika ilitengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji.
Via>>BBC
Theme images by rion819. Powered by Blogger.