Utafiti: KERENGENDE WA KIKE HUJIUA KUKWEPA KUFANYA MAPENZI


Utafiti mpya umebaini kwamba kerengende wa kike huwa anajifanya kuwa amekufa ili kukwepa wenzao wa kiume.

Rassim Khelifa, kutoka chuo kikuu cha Zurich Switzerland, anasema kwamba aliona kerengende wa kike aliyekuwa akifuatwa na wa kiume ili kufanya mapenzi, akijiangusha na kulala kana kwamba amefariki, hadi pale kerengende wa kiume anapoondoka.

Ripoti hiyo imechapishwa kwenye jarida la ikolojia.

Bwana Khelifa amsema kuwa kerengende wa kike hunyanyaswa kwa sababu huwa hawana ulinzi baada ya kutaga mayai ikilinganishwa na kerengende wengine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527