MAJAMBAZI YAUA MFANYABIASHARA BAADA YA KUKOSA PESA DUKANI

RPC TANGA- BENEDICT WAKULYAMBA
**
MFANYABIASHARA Mohamed Ally mkazi wa kijiji cha Kwekivu wilayani Kilindi Mkoani Tanga, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi ambao walivamia dukani kwake usiku.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, alisema tukio hilo limetokea juzi katika kijiji hicho ambapo majambazi hao wanaokadiliwa kuwa wanne walivamia duka la mfanyabiashara huyo wakiwa na silaha za moto, mapanga na marungu kwa lengo la kupora fedha.

Alisema majambazi hao baada ya kuvamia duka hilo walimlazimisha mfanyabiashara huyo kutoa fedha ambapo aligoma na hivyo majambazi hao waliamua kufanya msako wa kutafuta fedha ndani ya duka lakini wakakosa.

Baada ya kukosa fedha hizo waliamua kumpiga risasi ubavuni na hatimae kusababisha kifo cha mfanyabiashara hiyo. 

Jeshi la Polisi linaendelea na msako waliofanya tukio hilo.
Chanzo-zanzibarnikwetu blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post