Utafiti: HIZI NDIYO FAIDA ZA KUTEMBEA NA KUKIMBIA

Inafahamika wazi kuwa kutembea na kukimbia ni sehemu nzuri sana ya kuimarisha afya ya moyo, na mara nyingi madaktari na wataalamu wa afya wamekuwa wakitoa ushauri wa kufanya aina hizo za mazoezi.

Utafiti mpya pia umebainisha kuwa matendo hayo; kutembea na kukimbia husaidia kwa kiwango kikubwa kuufanya ubongo ufanye kazi yake vizuri huku wataalamu wakidai kuwa matokeo ya mguu kukanyaga ardhi hutuma mawimbi ya presha ambayo hufungua zaidi mishipa ya damu ambayo husaidia kuongeza kiwango cha usambazaji wa damu kwenye ubongo.

Watafiti kutoka New Mexico Highlands University walifanya uchunguzi wa usambazi wa damu kwenye ubongo kwa wazee 12 wakiwa wamepumzika, kusimama na wakiwa wanatembea na kubaini kuwa kutembea na kukimbia hutengeneza presha ya mawimbi ambayo yaliongeza usambazaji wa damu ubongoni.


Ilidhaniwa mwanzo kuwa usambazaji wa damu kwenye ubongo hufanywa bila kutegemea akili ya mtu kunakofanywa na mwili na kuathiriwa na mabadiliko kwenye damu.

Watafiti hao waliandika kwenye utafiti wao: “Data mpya zinasema kuwa kusambaa kwa damu kwenye ubongo kuna nguvu sana. Kutembea na kukimbia kunaweza kuongeza mzunguko wa damu na utendaji kazi wa ubongo wakati wa mazoezi.”

Utafiti huu umekuja siku chache baada ya watafiti kutoka Iowa State University kubaini kuwa kila saa ya kukimbia inaweza kuongeza muda wa kuishi kwa saa saba bila kujali unakimbia namna gani na kwa umbali gani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post