RAIS MAGUFULI AFUTA AJIRA ZA WATUMISHI WA UMMA 9,932 WENYE VYETI FEKI

Rais Dk. John Pombe Magufuli, ameiagiza Wizara ya Fedha kufuta mara moja ajira za watumishi wa umma 9,932 waliobainika kughushi vyeti, kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma.


Akiongea leo mara baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mjini Dodoma, Rais Magufuli pia amewataka watumishi hao kuondoka wenyewe na iwapo watakaidi wakamatwe na vyombo vya dola na kushtakiwa.

Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.

Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema, kwa Mujibu wa Kanuni na Sheria za nchi zinabainisha wazi kuwa mtu atakaebainika kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha Jela.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527