POLISI WATUMIA SILAHA KUWATAWANYA WAFANYABIASHARA MWENGE DAR

Jeshi la Polisi limetumia silaha za moto kuwatawanya wafanyabiashara katika eneo la Mwenge, wilayani Kinondoni leo.

Taharuki iliwakumba wakazi wa eneo hilo mara baada ya polisi hao kuanza kuwatanya wafanyabiashara hao waliofunga barabara wakishinikiza magari yaruhusiwe kupaki katika eneo hilo.


Inaelezwa kuwa polisi wamezuia watu kupaki magari katika eneo hilo hali iliyosababisha wafanyabiashara hao kutofungua biashara zao leo.

Mmoja wa wafanyabiashara na shuhuda wa tukio hilo, Musa Godwin alisema polisi walifika sokoni hapo saa12 asubuhi na kutawanya wafanyabiashara waliofunga barabara kuzuia polisi magari yasiegeshwe eneo hilo.


"Walifika hapa sokoni saa 12 asubuhi na baadhi ya watu walifunga njia ikasababisha polisi wapige risasi hewani, hadi sasa wanazunguka hapa kuzuia magari ambao ni wanunuaji wetu," alisema Godwin.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post