MAUAJI YA POLISI YAMTOA MACHOZI MHUBIRI KANISANI SHINYANGA

MHUBIRI wa Kanisa la IEACT lililoko Manispaa ya Shinyanga, Eliamani Kisanaga, amebubujikwa na machozi kutokana na vitendo vya kinyama vinavyoendelea hapa nchini vya kuuawa kwa polisi.


Kutokana na hali hiyo, aliwashauri Watanzania kumrudia Mungu kwa kuishi kwa kupendana kama alivyoagiza katika vitabu vitakatifu. Mhubiri huyo alitokwa na machozi wakati wa Misa ya Pasaka, iliyofanyika juzi, kwenye kanisa hilo. Pia alitumia fursa hiyo kuwaaga waumini wa kanisa hilo kuwa anahama. 

"Tuishi kama Kristu kwa kuiga matendo yake, tusijiite Wakristu tu bila matendo, huko ni kujidanganya kwani hakuna kitabu kinachohubiri kuua, hiyo ni njia ya shetani. Tunakokwenda Watanzania wenzagu ni kwenye laana," alisema. 


Aliongeza: "Nchi yetu katika sura ya kimataifa, tulikuwa na sura nzuri ya amani na upendo, lakini ghafla yakaanza mauaji ya vikongwe, mauaji ya walemavu wa ngozi, dawa za kulevya na leo tunaua askari wetu wanaotulinda, tunakwenda wapi?" 

Pia, aliwataka Wakristo kuishimaisha mema na kuwa mfano kwa watu wengine ambao si wakristo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post