JINSI UNAVYOSHIKA SIMU NDIVYO UNAVYOWEZA KUIBIWA NAMBARI YAKO YA SIRI 'PIN NUMBER'

Ni rahisi programu mbaya kupata data yako na maelezo yako ya kibinafsi

Jinsi unavyoishika simu yako unapoitumia inaweza kuwapa wadukuzi nafasi ya kuiba nambari yako ya siri au 'pin number', kulingana na utafiti uliofanywa.

Wataalam katika chuo kikuu cha Newcastle walichambua jinsi watu walivyozishika simu zao wakati walikuwa wakiweka nambari zao za siri na wanasema waliweza kutambua kwa usahihi wa asilimia 70 nambari zote za siri zenye tarakimu nne baada ya kujaribu mara moja tu na kwa asilimia 100 baada ya kujaribu mara tano.

Wataalam hao wa maswala ya teknolojia wanasema makampuni ya teknolojia yanayofahamu tatizo hili lakini hawajui watafanya nini.

Dkt. Maryam Mehrnezhad kutoka shule ya kompyuta sayansi ya chuo hicho amesema: "Simu nyingi aina ya 'smartphones' na 'tablets' zimewekwa sensa.

Lakini kwa kuwa tovuti nyingi na programu za simu haziulizi ruhusa kabla ya kutumia propgramu hizi, ni rahisi sana kwa programu mbaya kupata data."

Dkt Mehrnezhad anasema kuwa: "Ukifungua kurasa kwenye baadhi ya tovuti ambazo zina programu hizo mbaya ukitumia simu yako, kisha ufungue tovuti nyingine, ile ya kwanza ina uwezo wa kunakili maelezo yote ya kibinafsi unayotoa.Hakuna kampuni ya teknolojia iliyopata suluhu ya tatizo la programu zinazoiba data muhimu

"Na jambo baya zaidi ni kuwa usipofunga kurasa hizo, programu hizo zinaweza kupeleleza hata simu iwapo simu imewekwa nambari ya siri.

Watu wanashughulika sana na kamera na programu inayoonyesha ramani, GPS kuliko sensa hizo.

Wataalamu hao wamegundua kwamba kila unachofanya katika simu iwe ni kupiga simu, kuandika ujumbe au kutafuta kitu hupelekea mtu kuishika simu kwa njia fulani ya kipekee.

Kwa hivyo kwenye tovuti inayofahamika, waliweza kujua mtu amefungua ukurasa upi na nini alichokuwa akiandika, kulingana na jinsi alivyoishika simu.

Wanasema wameelezea kampuni zote kuu za teknolojia kama Google na Apple kuhusu hatari hii lakini hakuna aliyeweza kutoa suluhu hadi sasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post