Audio & Picha - JESHI LA POLISI SHINYANGA LILIVYOJIPANGA KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA PASAKA


Katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka,Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limejipanga kikamilifu kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu hivyo limetaka wananchi nao kujipanga kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa jeshi la polisi mkoa,leo Alhamis Aprili 13,2017,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema vitendo vya kihalifu havina nafasi mkoani humo.

“Kuanzia leo sisi tumeongeza jitihada za kuimarisha usalama katika maeneo ya usalama barabarani,makanisani na maeneo mengine yote yanayohitaji ulinzi”,ameeleza.

“Naomba familia zote ziache maeneo ya nyumbani yakiwa salama,wasiondoke kwenda kusherekea sikukuu ya pasaka bila kuacha watu wa kuangalia familia...sisi tutakuwepo katika maeneo yote mtaani kuhakikisha kuwa wananchi wanasherehekea sikukuu kwa amani”,amesema kamanda Muliro.

Aidha amesema jeshi hilo la polisi limepiga marufuku disko toto katika kumbi zote za starehe.

MSIKILIZE HAPA KAMANDA MULIRO AKIZUNGUMZA LEO


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 13,2017 katika ukumbi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza ukumbini ambapo amesema jeshi hilo pia linaendelea na operesheni kubwa ya dawa za kulevya na uzuiaji na ukamataji wa pombe zinazohifadhiwa katika vifungashio vya plastiki maarufu ‘Viroba’
Gari la maji ya kuwasha likitoka katika kambi ya jeshi la polisi mjini Shinyanga leo Aprili 13,2017 ambapo mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ameshuhudia msululu wa magari ya polisi yakipita katika mitaa mbalimbali mjini Shinyanga
Askari polisi wakiwa kwenye gari
Magari ya polisi yakiwa barabarani
Magari ya polisi yakiwa barabarani
Magari ya polisi yakiwa mtaani

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post