KAULI YA WAZIRI WA HABARI NAPE NNAUYE KUHUSU MADAI YA MAKONDA KUVAMIA CLOUDS MEDIA NA ASKARI WENYE SILAHA

Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye amesema kuwa kesho Machi 20, 2017 atakwenda katika Ofisi za Clouds Media Group kujua kilichotokea baada ya kuwapo taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa ofisi hizo zilivamiwa.


Taarifa hizo zinadai kuwa ofisi za Clouds Media Group zilizopo Mikocheni B Dar es Salaam, zilivamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Usiku wa Machi 17 mwaka huu.

Taarifa hizo ambazo hazijathibitishwa bado zinaenda mbali zaidi na kudai kuwa, RC Makonda alikuwa ameambatana na Askari wakiwa na silaha ambapo aliwashinikiza watangazaji wa kipindi cha De Weekend Chat Show kurusha mkanda wa video aliorekodiwa mwanamke mmoja na anayedai kuwa alizaa na Askofu Gwajima.

Waziri Nape amesema kuwa yeye kama kiongozi mwenye dhamana na tasnia ya habari, atakwenda ili afahamu ukweli wa mambo kuhusu hasa kilichotokea.……

“Kesho asubuhi kama Waziri Mwenye dhamana na HABARI nitatembelea CloudsMedia kujua kilichotokea.Nawaomba sana wanahabari nchini KUTULIA kwasasa”==> Video iliyosambaa 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post