JAJI AMUULIZA MWANAMKE ALIYEBAKWA "KWANINI HAKUBANA MAPAJA WAKATI WA TUKIO"


Jaji mmoja kutoka Canada aliyemuuliza mwanamke katika kesi ya ubakaji ''kwa nini hakuweka mapaja yake pamoja'' wakati wa tukio hilo amejiuzulu.

Robin Camp alijiuzulu baada ya kamati ya nidhamu kupendekeza kuwa afutwe kazi.

Bwana Camp alisema kuwa alisikitishwa na matamshi yake lakini jopo la nidhamu lilisema liliona matamshi yake yalikosa hali ya kutopendelea na heshima.

Waziri wa haki katika jimbo hilo amekubalia kujiuzulu kwake.

Matamshi ya bwana Camp yaliotolewa wakati wa keshi ya ubakaji mwaka 2014 yalizua hisia kali na kusababisha ukosoaji mkali kutoka kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono pamoja na mawakili wao.Jaji huyo alichukua msimamo na kuliambia baraza hilo kwamba alifahamishwa kuhusu makosa yake na kwamba aliomba msamaha juu ya matamshi yake.

Baraza hilo ambalo husimamia idara ya haki lilibaini kwamba vitendo vya bwana Camp wakati wa keshi hiyo vilikuwa na uharibifu wa wazi kuhusu sera ya kutoa haki katika idara hiyo na kwamba hawezi kuendesha tena afisi hiyo.

Pia ilibainika kwamba jaji huyo alizungumza na mlalamishi kwa lugha isioheshimika inayofedhehesha na kuonyesha ubabe.
Chanzo-BBC


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post