MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE AKAMATWA NA POLISI


Leo Jumatatu Februari 20, 2017 Kamishna wa kanda maalumu Dar es salaam Simon Sirro amethibitisha kukamatwa kwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo “CHADEMA”.


Hata hivyo msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene, amesema Freeman Mbowe amekamatwa wakati akiwa njiani kuelekea kituo cha polisi kwa mahojiano kuhusiana na sakata la dawa za kulevya baada ya polisi kumtaka afike polisi. 

Jioni ya Jumatatu Mbunge huyo wa Hai Kilimanjaro alichukuliwa na Polisi kwenye msafara wa magari yasiyopungua matatu ambapo iliripotiwa baadae kwamba Polisi walikwenda kufanya upekuzi kwenye nyumba zake Kawe na Mikocheni kwa mujibu wa Afisa habari wa CHADEMA.

Msemaji huyo wa CHADEMA Tumaini Makene alithibitisha Polisi kupekua nyumba zake na kuandikisha maelezo ya majirani ambapo akasema kwenye mida ya saa sita usiku huu Polisi wamemrudisha Mbowe kwenye kituo cha Polisi kati na wamemfungulia jalada la Uchunguzi…..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527