MUME AMUUA MKE WAKE KWA NYUNDO NA KISU KISHA KUJIUA DAR AKIACHA UJUMBE MZITO

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mudi Kuchunga mkazi wa Boko amemuua mke wake Mama Ziada kwa kisu na nyundo na kisha kujinyonga usiku wa kuamkia jana akiacha ujumbe mzito wa dhamira ya kufanya hivyo upelekwe kwa mamlaka za polisi serikali za mitaa na majirani wote.


Tukio hilo lilivuta hisia za watu na hasa katika ujumbe aliouacha kuonyesha michoro ya zana alizotumia kumuua mkewe pamoja na kuomba tukio hilo lisimuhusishe mtu yeyote kuwa ameamua kuua mwenye kwa sababu za ndani ya mahusiano yao wenyewe na akisistiza ujumbe huo usomwe kwa umakini.





Hata hivyo jeshi la polisi walifika katika eneo la tukio na kuchukua miili hiyo na barua zote zilizoandikwa kuhusiana na tukio hilo, ikiwemo michoro ya vifaa alivyotumia kuua, nyundo na kisu huku viongozi wa serikali eneo ya mtaa na kata wakilaani na kueleza hisia zao kwa tukio hio.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527