MBUNGE APATA AJALI AKIWA KWENYE ZIARA NA NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA MKOANI MANYARA


Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.


Baada ya ajali hiyo kutokea mbunge Paulina Gekul ambaye ni mbunge wa Babati mjini alikimbizwa hospitali ya mkoa wa Manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hicho na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo. 

Hata hivyo baada ya ajali kutokea Naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa Babati huku Mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa Babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwa ajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.
Chanzo-Mpekuzi blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post