Makubwa Haya!! WACHAWI WAFANYA MATAMBIKO KUMWONDOA TRUMP MADARAKANI


Kadi za wachawi

Wapinzani wengi wa rais wa Marekani Donald Trump, wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka minne ili aweze kuondoka madarakani.

Lakini wachawi nchini Marekani hawakubaliani na hilo.

Usiku wa manane siku ya Ijumaa, wale wanaoamini uchawi kote nchini Marekani, waliandaa matambiko yenye nia ya kumuondoa Trump uongozini.

Hadi sasa ukurasa wa Facebook wa matambiko huyo umepata wafuasi 10,500.
Hatua hizo zimezua ghadhabu kotoka kwa wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao kwa kutangaza vita vya kiroho.

Wachawi hao wanapanga kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini. Tambiko lingine litafanyika Machi 26.

Chama cha wakiristo nacho kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili uchawi huo.

Hata hivyo Trump hajazungumzia lolote kuhusu vita hivyo kati ya kanisa na uchawi.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527