BABU WA MIAKA 68 ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA AKILIMZEE mwenye umri wa miaka 68 ametupwa jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mtoto mwenye ulemavu wa akili.

Mzee huyo, Nadhan Kifaru alitiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashitaka wa Polisi, Godwin Ikema kuwa mtuhumiwa alimbaka binti huyo mwenye umri wa miaka 13, Desemba 9, 2016 katika kijiji cha Makutupa wilaya ya Mpwapwa , Dodoma Kesi hiyo ya jinai namba 123 ya mwaka 2016 ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Paschal Mayumba.

Alipopewa nafasi ya kujitetea mzee huyo alisema yeye kutokana na umri wake wa miaka 68 hana nguvu tena za kushiriki tendo la ndoa kwa hiyo hawezi kubaka na amefikishwa mahakamani kwa chuki za wanakijiji.

Hata hivyo, hakimu Mayumba alimueleza kuwa mahakama hiyo imetia hatiani na kumtaka ajitetee ili mahakama isimpe adhabu kali.

Mshitakiwa huyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana yeye kuwa mzee wa miaka 68 na kwamba anakabiliwa na ugonjwa wa pumu ambao hawezi kukaa gerezani.

Akimsomea hukumu hiyo hakimu Mayumba alisema kutokana na mahakama kumuona na hatia pamoja na kuzingatia utetezi wake inampeleka jela miaka 30.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post