WATU 39 WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKISHEREHEKEA MWAKA MPYA 2017Takriban watu 39 wakiwemo wageni 15 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la klabu ya burudani mjini Istanbul Uturuki, kulingana na waziri wa maswala ya ndani nchini humo.

Mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakijiburudisha katika mkahawa huo wa Reina saa saba usiku wakati ambapo watu walikuwa wakisherehekea kuingia kwa mwaka mpya.

Waziri huyo S├╝leyman Soylu ameelezea waliojeruhiwa kuwa 69 .

Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.

Baadhi yao iliwabidi kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia.

Polisi mmoja ni miongoni mwa waliofariki.

Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika wa shambilo hilo hajakamatwa bado.

Chanzo-BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post