ALIYEWEKA NYAMA YA NGURUWE MSIKITINI AFARIKI DUNIA



Mtu aliyeweka nyama ya nguruwe katika mlango wa msikiti nchini Uingereza amefariki akihudumia kifungo cha miezi 12 jela.

Kevin aliweka vipande vya nyama ya nguruwe katika mlango wa msikiti wa Jamia huko Totterdown.

Kevin Crehan alihukumiwa kifungo hicho katika mahakama ya Bristol Crown mnamo mwezi Julai kwa kuchochea machafuko ya uma.

Msemaji wa hudumu za jela hiyo amethibitisha kuwa Kevin mwenye umri wa miaka 35 alifariki siku ya Jumanne lakini akaongezea kuwa uchunguzi unaendelea.

Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa.

Jela hiyo imekataa kutoa maelezo yoyote ya sababu ya kifo chake.
Chanzo-BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post