MVUA YA DAKIKA 10 YAZUA BALAA SHINYANGA ,NYUMBA ZAIDI YA 40 ZAEZULIWA NA UPEPO MKALI


Hapa ni katika shule ya MsingiViwandani iliyopo katika manispaa ya Shinyanga. 

Mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika manispaa ya  Shinyanga imeleta madhara baada ya zaidi ya nyumba 40 kuezuliwa mapaa na nyingine kuanguka huku watu 19 wakijeruhiwa.

Mvua hiyo imenyesha usiku wa Januari 11,2017 majira ya saa nne usiku.

“Mvua hii ilikuwa na upepo mkali sana pamoja na mawe baada ya kuona nyumba yangu inaanza kumomonyoka vipande vipande ikabidi ni chukue watoto wangu kwenda nje mara kidogo nyumba yote ikashuka chini na hivyo kusalimika na watoto wangu",amesema mmoja wa waathirika wa mvua hiyo aliyezungumza na Malunde1 blog.

Diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri (CCM) amefika katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na kujionea uharibifu uliojitokeza kufuatia mvua hiyo inayodaiwa kunyesha kwa muda takribani dakika 10 tu majira ya saa nne usiku wa Jumatano Januari 11,2017. 

Diwani huyo amesema mvua hiyo mbali na kuharibu nyumba zaidi ya 40 pia madarasa manne na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Viwandani zimeezuliwa.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi viwandani iliyopo mjini Shinyanga Matiku Lukanga amesema katika shule hiyo vyumba vinne vya madarasa, vyoo vyote na ofisi ya walimu vimeezuliwa mapaa yao, na kuharibu vitabu vya kufundishia.

Kamanda wa jeshi la polisi mkaoni Shinyanga Jumanne Murilo amesema sehemu ambazo zimepata maafa ya mvua hiyo kuwa ni kata ya Ibadakuli,Kitangili na Kizumbi.

Jeshi la zimamoto limefanya jitihada za kuokoa mali mbalimbali 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post