Picha: MAZISHI YA PADRE ANDREW LUPONDYA NA WATOTO WATANO WA KAHAMA WALIOFARIKI AJALINI


Maaskofu wa majimbo manne , mapadri , watawa na mamia ya waamini wameshiriki misa ya mazishi ya Padri Andrew Lupondya (33) na watoto watano wa Shirika Rafiki wa Utoto wa Yesu (VIFRA) na mlezi wao Mama Judith Kajwahula (63 ) wa Jimbo Katoliki Kahama waliofariki katika ajali ya gari.

Ajali hiyo ilitokana na gari walilokuwemo kugongana uso kwa uso na roli aina ya fuso Desemba 24, saa 9 mchana na marehemu walizikwa jana katika eneo la Kiwanja cha Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga, Parokia ya Kahama Mjini mkoani Shinyanga.

Misa ya mazishi imefanyika jana katika Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Kahama na imeongozwa na Askofu Fravian Kasala wa jimbo Katoliki Geita, pamoja na Maaskofu Liberatus Sangu wa Shinyanga, Joseph Mlola wa Kigoma na mwenyeji Askofu Ludovick Minde wa jimbo Katoliki la Kahama.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post