TANGAZO MUHIMU KWA WAMILIKI WA BLOGS TANZANIA

Taarifa kwa Wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Chama cha wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (Bloggers) kinawajulisha kuwa TBN imeandaa semina na mkutano Mkuu kwa wanachama wake utakao fanyika tarehe 5 na 6 ya mwezi Desemba 2016 jijini Dar es Salaam.


Semina na mkutano huo kwa Bloggers wa TBN utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya PSPF Dar unatarajiwa kujumuisha wanachama wote wa Tanzania Bara na Visiwani.

TBN inawaomba wanachama wake wote kushiriki katika semina na mkutano huo bila kukosa. Wana TBN watakaoshiriki wanaombwa kuthibitisha ishiriki wao kwa uongozi wa TBN kwa kutuma SMS kwa namba zifuatazo 0717 030 066 au 0713 052 828 ama email;- mushijoa@gmail.com (unapothibitisha taja jina kamili Blogu na mkoa unaotoka). 

NB;- Kwa bloggers wa kutoka mikoani na Zanzibar, TBN itagharamia usafiri wao na malazi kwa hoteli zilizopangwa kwa siku mbili. 

Tafadhali kabla ya kuanza safari unatakiwa kufanya mawasiliano na Mwenyekiti, Katibu & Mhadhini wa TBN. 

Pia unatakiwa kufika Jijini Dar ES Salaam tarehe 4/12/2016.

TBN itagharamia malazi kwa siku mbili tu. 

Asanteni na karibuni. 

Imetolewa na Kamati tendaji ya TBN taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527