Picha: MAZISHI YA SPIKA MSTAAFU SAMWEL SITTA URAMBO TABORA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora akieleke Urambo kuhudhuria mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta, Novemba 12, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na Viongozi wa Serikali wa mkoa wa Tabora, Viongozi wa Vyama vya siasa na dini baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora akiwa njiani kwenda Urambo kwenye mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tabora. Wote walikuwa wakienda Urambo kushiriki mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta.
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu, Spika Mstaafu Samuel Sitta, Urambo mkoani Tabora ambako alishiriki mazishi 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mjane wa marehemu Spika Mstaafu, Samuel Sitta baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu, Urambo Tabora kwa mazishi 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wanafamilia na ndugu wa marehemu Spika Mstaafu, Samuel Sitta bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Urambo mkoani Tabora kwa mazishi 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wanafamilia na ndugu wa marehemu Spika Mstaafu, Samuel Sitta bada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Urambo mkoani Tabora kwa mazishi 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Busega na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani ambaye sasa ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Simiyu katika mazishi ya Spika Mstaafu Samuel Sitta yaliyofanyika Urambo Tabora, Novemba 12, 2016. Kulia kwake ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto kwake ni Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba katika mazishi ya Spika Mstafu, Marehemu Samuel Sitta, Urambo mkoani Tabora
Maaskofu na wachungaji wakiuombea mwili wa Spika Mstaafu, Marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yaliyofanyia Urambo Tabora.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta kabla ya mazishi yake yaliyofanyika Urambo mkoani Tabora
Bibi Kagoli Fundikira ambaye ni Mama Mzazi wa Spika Mstafu , marehemu Samuel Sitta akiongozwa na Mgalula Fundikira kwenda kwenye kaburi la mwanae katika mazishi yaliyofanyika Urambo.
Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu, na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipoteremshwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika urambo, Tabora.
Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu, na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipokuwa ukiteremshwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Tabora.
Mjane wa Marehemu Spika Mstaafu, Margareth Sitta, Mama Mzazi wa marehemu, na watoto wa marehemu wakigusa jeneza na kushuhudia wakati mwili wa marehemu Samuel Sitta ulipoteremshwa kaburini 
Bibi Kagoli Fundikira ambaye ni Mama Mzazi wa marehemu Spika Mstaafu Samuel Sitta akitupa udongo kwenye kaburi la mwanane katika mazishi yaliyofanyika Urambo, Tabora 
Mama Margareth Sitta ambaye ni Mjane wa marehemu Spika mstaafu, Samuel Sitta akitupa udongo kwenye kaburi la mumewe katika kazishi yaliyofanyika Urambo 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakitupa udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi yaliyofanyika Urambo 
Viongozi wa Vyama vya siasa na serikali pamoja na wanafamilia wakiweka udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta katika mazishi yaliyofanyika Urambo.
Maaskofu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta wakiweka shada la maua kwenye kaburi katika mazishi yaliyofanyika Urambo.
Mama Margareth Sitta ambaye ni mjane wa Spika Mstafu, marehemu Samuel Sitta akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe katika mazishi yaliyofanyika Urambo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta 
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu, marehemu Samuel Sitta
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na familia ya Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta baada ya mazishi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na familia ya Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta baada ya mazishi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na familia ya Spika Mstaafu marehemu Samuel Sitta baada ya mazishi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na maaskofu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na maaskofu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Spika Mstaafu, Samuel Sitta. Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akimpa pole Mama wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta, Hajjat Zuwena Fundikira.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akimfariji Mjane wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta Mama Magreth Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta wakati wa mazishi wa Spika huyo Mstaafu. Anayefuatia ni Mkuu wa Kambi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Y. Ndugai akitoa salama za rambirambi wakati wa mazishi wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akiweka shada la maua katika Kaburi la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akiweka shada la maua katika Kaburi la aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta.
Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post