BASI LA SAFARI NJEMA LAGONGANA NA LORI NA KUWAKA MOTO,MTU MMOJA AFARIKI,MAJERUHI 20 (Picha + Video)


Basi lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kwenda jijini Dar es salaam, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement  lenye namba zake za usajili  namba ya usajili 534 BYJ jioni ya leo Jumapili October 30 2016.


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa na kuna taarifa kuwa mali zote zilikowemo katika
basi vimeteketea kabisa kwa moto.Lori likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana  kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili  kuwaka moto


Baadhi ya Wakazi wa eneo la Kimara Stop Over na Kimara Suka wakielekea kushuhudia eneo la ajali kati ya basi la Safari Njema na Lori lililokuwa limebeba shehena kubwa ya mifuko ya Cement.


Baadhi ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza kuondoka na mifuko ya Cement iliyokuwa imebebwa na lori hilo.
Angalia video hapa chini Basi la Safari Njema likiteketea kwa moto

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post