UMESIKIA HABARI YA KABURI KUFUKULIWA NA KUKUTWA VITU VYA AJABU ZANZIBAR?? HUU HAPA NDIYO UKWELI


Kumekuwa na taarifa iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba Wakazi wa Jumbi, Wilaya ya kati Unguja wiki mbili baada ya mazishi ya mtu mmoja kugundua kuwa mtu aliyezikwa yupo mtaani na anaonekana katika mazingira ya kutatanisha, na hivyo kuamua kwenda kulifukua kaburi na kukutana na majanga hayo hapo kama picha zinavyoonesha.

Tumefuatilia suala hili kwa undani zaidi inasemekana taarifa hizo hazina ukweli lakini taarifa iliyo sahihi ni kwamba,
taarifa ya kufukuliwa kaburi imetokea Bungi na siyo Jumbi kama ilivyodaiwa.


Hata hivyo hakuna mtu aliyekufa na kuzikwa kisha kuonekana mitaani kama taarifa zinavyosema.


Kilichotokea ni kwamba wametokea watu wasiojulikana wameenda porini kisha kuchimba shimo mfano wa kaburi na kuzika vitu vinavyosadikiwa kuwa vya ushirikina.


Shimo lilifukuliwa chini ya usimamizi wa polisi na maafisa wengine wa kiserikali na hakupatikana mtu aliyezikwa hapo.Chanzo-http://www.zanzinews.com/

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post