HII NDIYO NDEGE YENYE UBORA ZAIDI NA STAREHE ZA KUTOSHA KULIKO YOYOTE DUNIANI

Nimeipata hii ya Ndege inayotajwa kuwa na starehe za kutosha ikiwa imetengenezwa ubora kuliko Ndege yoyote ile duniani. Ndege hii inafahamika kama “World’s Most Luxurious Commercial Jet ikiwa na jina la kibiashara Crystal.

Crystal Plane ina mgahawa wa kisasa zaidi kuliko hata migahawa ya mitaani, Bar ambayo ni Classic sana, pamoja na huduma ya Internet yenye kasi zaidi ya Wi-Fi… Ndege hii inamilikiwa na kampuni kutoka nchini Marekani.

Gharama za kuikodi ndege hii ni dola za Marekani elfu hamsini kwa siku moja huku abiria akipewa huduma ya hadhi ya hoteli ya five star. Ndege hii inatarajiwa kuanza kutumika na wateja ifikapo mwaka 2017.

Nimekusogezea hapa picha za ndani ya ndege hiyo mtu wangu.















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527