Mwanamke mmoja nchini Vietnam amekiri kutoa mguu na sehemu ya mkono wake vikatwe ili aweze kudai malipo ya bima, kwa mujibu wa polisi. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 , anayetambuliwa kama ”Ly Thi N”, alidanganya kuwa aligongwa na treni, limeripoti gazeti la polisi nchini Vietnam.
Lakini kwa sasa ameripotiwa kukiri kwamba alimlipa rafiki yake dola $2,200 (sawa na zaidi ya shilingi milioni 44 za kitanzania) akate viungo vyake.
Lengo lilikuwa ni kudai dola zaidi ya $150,000 (sawa na zaidi shilingi 300,000,000/- za kitanzania) kutoka kwa kampuni ya bima yake.
Kwasasa mwanamke huyo akiwa amepona majeraha yake. anaendesha biashara kwa shida, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
Social Plugin