Yanga Yakubali Kichapo cha Bao 3-1 Kutoka Medeama Mjini Takoradi -Ghana



Julai 26, 2016 ilikuwa ni siku nyingine kwa wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa nne wa Kundi A Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana.


Yanga wamecheza mchezo wao wa nne dhidi ya Medeama mjini Takoradi Ghana na kukubali kipigo cha goli 3-1, kipigo ambacho kimezidi kufifisha safari ya Yanga kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, magoli ya Medeama yamefugwa na Daniel Amoah dakika ya 7 na Abbas Mohammed aliyefunga magoli mawili dakika ya 22 na 37.



Simon Msuva ndiyo aliyefunga goli la kufutia machozi kwa Yanga kwa mkwaju wa penati dakika ya 24, kwa matokeo hayo Yanga wanaendelea kusalia na michezo miwili dhidi ya MO Bejaia ya Algeria watakaocheza nyumbani na TP Mazembe ya Kongo watakaocheza ugenini, nafasi ya Yanga kufuzu katika hatua ya nusu fainali ni finyu sana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post